
Manchester City ni mabingwa Uingereza
Manchester City ndio mabingwa wa ligi kuu ya Uingereza msimu huu.
Vijana wa Manuel Pelligrini walitawazwa mabingwa
katika siku ya mwisho ya ligi kuu ya Uingereza baada ya kuilaza West
Ham mabao 2-0.Umati uliojaa uwanjani Etihad ulimiminika uwanjani baada ya kipenga cha mwisho.
Kocha huyo kutoka Chile alifaidika na kichapo cha Liverpool mikononi mwa Chelsea na hivyo alihitaji sare ya aina yeyote kujihakikishia ushindi.
Mancity iliititima West ham 2-0 na kutamatisha msururu wa mechi tano bila ya kushindwa .
Pelligrini, atakumbukwa kwa kuirejesha kombe Etihad baada ya Roberto Mancini kupigwa kalamu kwa kushindwa kutetea taji msimu uliopita .
Kocha huyo mwenye miaka 60 anajivunia mabao 102.
Kwa upande wao Liverpool walisajili ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Newcastle United uwanjani Anfield.
ARUSO